![]() |
| Watu wakiwa wamekusanyika kwenye eneo la mlipuko katika mtaa wa biashara wa Karrada mjini Baghdad, nchini Iraq, Julai 3, 2016. |
Watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa katika
milipuko miwili iliyotokea katika eneo la soko maarufu mjini Baghdadi nchini
Iraq usiku wa kuamkia leo, kituo cha televisheni cha al-Sumaria mimeripoti.
Polisi na maafisa wa afya wameliambia shirika la habari
la Reuters kuwa idadi ya waliofariki dunia inafikia 80.
Kundi la Daesh (ISIS) limedai kuhusika na mlipuko huo wa
kujitoa mhanga lililotokea katika eneo la Karrada kupitia taarifa yake
mtandaoni.
Bomu hilo lililopandikizwa kwenye gari lililipuka jirani
na mgahawa mmoja katika eneo hilo na kuua watu kadhaa huku wengine 20
wakijeruhiwa.
Video iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii imeonesha
moto mkubwa kutoka mtaa huo wa Karrada uliotokana na mlipuko huo.
Mlipuko wa pili ulitokea katika eneo la al-Shaab, ambalo
lina wakazi wengi wa madhehebu ya Kishia kaskazini mwa mji mkuu wa Iraq na
kusababisha vifo na majeruhi ya watu kadhaa, kituo hicho kimesema.
Mwezi uliopita, vikosi vya Iraq viliwafurusha wanamgambo
wa kundi la Daesh kutoka mji wa Falluja uliopo magharibi mwa Baghdad, ambao
ulikuwa ngome yao iliyotumika kama kitovu cha uratibu wa mashambulizi hayo.

0 comments:
Post a Comment