
Maisha ya kijana Albert (39) yalibadilika moja kwa moja
baada ya kupata maradhi ya saratani yaliyosababishwa na steroidi na vinywaji
vya kuongeza nguvu ambavyo alikuwa akivitumia ili kupata mwili wenye misuli
mikubwa ambao atajivunia mbele ya watu, lakini akapata kitu ambacho
hakukitarajia.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Albert
alikuwa na mwili mkubwa na misuli maridhawa, akataka kuwa kiigizo kwa vijana
wanaotembelea maeneo ya mazoezi (gym), lakini kwa masikitiko makubwa ndoto yake
ya kuwa shujaa mwenye mwili mkubwa iliishia kuwa simulizi yenye kuhuzunisha
sana. Sasa badala ya kuhamasisha matumizi ya madawa yanayoongeza misuli, akawa
mpingaji mkubwa wa madawa hayo.

Miaka kadhaa baadaye, Albert alipatwa na saratani ya ini
kutokana na maada za kikemikali alizokuwa akizitumia kwa lengo la kukuza misuli
na kupunguza baadhi ya maeneo katika mwili wake, kwani ilithibtika kuwa maradhi
hayo yalitokana na matumizi hayo yaliyotajwa.
Albert alikuwa na mazoea ya kutumia kalori elfu 10 kwa
siku, kiwango ambacho kinachukuliwa kuwa ni kikubwa sana kwa mtu aliyebaleghe,
na kwa uchache alikuwa na mazoea ya kunywa kopo 8 za vinywaji vya kuongeza
nguvu ili vimsaidie katika ufanyaji wa mazoezi. Lakini Albert amefariki dunia
akiwa amekonda kutokana na maradhi ambayo yalimfanya apoteze uzito wote
aliokuwa ameupata.





UNGANA NA MZIZIMA 24:
Kupata habari na matukio kupitia WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment