![]() |
Miale ya radi ikiangaza wakati wa dhoruba ya usiku kwenye
mji wa badanari wa Guwahati, kaskazini mashariki mwa jimbo la Assam, India, Aprili
18, 2016.
|
Kwa uchache watu 67 wamepoteza maisha yao nchini India
kutokana na miale ya radi wakati mvua za msimu zikiikumba nchi hiyo, maafisa
wamesema.
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Majanga nchini humo
(NDMA), mmemetuko wa radi umewaua watu wasiopungua 47, wakiwemo wanawake na
watoto, wakati wa dhoruba ya radi iliyopiga usiku mzima katika maeneo
mbalimbali ya jimbo la Bihar Mashariki mwa India na kuwajeruhi wengine 22, hasa
katika maeneo ya mashambani.
“Tumethibitisha vifo vya watu 47 na tuna wasiwasi kuwa
idadi inaweza kuongezeka kutokana na ripoti mbalimbali kuendelea kumiminika
kutoka wilaya nyingine,” amesema Anirudh Kumar, ambaye ni afisa mwandamizi
katika wakala wa uratibu wa majanga katika Jimbo la Bihar.
Mashambulizi ya radi hutokea mara kwa mara katika jimbo
hilo katika kipindi cha pepo za msimu katika Bahari ya Hindi ambao huanza
katika wiki ya pili ya mwezi Juni mpaka mwezi Oktoba. Mvua za masika zilizoanza
mapema wiki hii zilikuwa za kwamba za msimu huo.
Wakati huo huo, mamlaka zinasema kuwa katika jimbo
jirani la Uttar Pradesh, lililopo maeneo ya kaskazini mwa India, kumeripotiwa
vifo vya zaidi ya watu 20 kutokana na mashambulizi ya radi katika kipindi cha
siku mbili.
Kwa mujibu wa ofisi ya Takwimu za matukio ya Uhalifu,
mwaka 2014, zaidi ya watu 2,500 walishambuliwa na radi na kufariki dunia.
Kila mwaka, miale ya radi hugharimu maisha ya maelfu ya
watu nchini India, wengi wao wakiwa ni wakulima wanaofanya kazi mashambani.

0 comments:
Post a Comment