![]()  | 
Picha hii iliyopigwa Aprili 3, 2015 inawaonesha askari
wa Nigeria wakifanya doria kwenye mji wa Malam Fatori baada ya mji huo ulio
kaskazini mashariki mwa Nigeria kukombolewa na vikosi vya Chad na Niger kutoka
mikononi mwa waasi wa Boko Haram. 
 | 
Vikosi vya majeshi ya Nigeria na Chad vimeanzisha
operesheni ya kijeshi ya pamoja dhidi ya kundi la Boko Haram kwenye mpaka wa
mataifa ya Niger na Nigeria.
Brigedia Jenerali Abdou Sidikou Issa, ambaye ni mkuu wa
kiufundi wa vikosi vilivyopo katika eneo lenye matatizo la Diffa la Nigeria,
amesema kuwa operesheni hizo zinaelenga kukomesha “udhibiti wa maeneo yote”
yalinayoshikiliwa na kundi hilo.
“Kazi yetu ni kuhakikisha usalama wa mpaka,” alisema.
Mataifa katika eneo hilo yameunda kikosi cha pamoja
chenye mchango mkubwa katika kuisaidia Nigeria kupambana na kundi hilo la
kigaidi.
Mapema mwezi Februari, mataifa manne yanayopakana na
Ziwa Chad ambayo ni Niger, Nigeria, Chad na Cameroon – yalianzisha operesheni
ya kijeshi ya pamoja kwa kushirikiana na kikosi maalum kutoka Benin, kwa lengo
la kukabiliana na kitisho cha wanamgambo wa Boko Haram katika eneo hilo.
Kundi la Boko Haram lilianza harakati zake za uasi mwaka
2009 kwa lengo la kuiangusha serikali kuu ya Nigeria.
Kundi hilo lilipanua mashambulizi yake mpaka kwenye mataifa
jirani, hasa o ambao unakadiriwa kugharimu maisha ya watu 17,000 na
kuwalazimisha wengine zaidi ya 2.6 kuyakimbia makazi yao.
Wanamgambo hao wamewateka nyara mamia ya vijana,
wanawake na watoto katika harakati yao ya miaka sita.
Utekaji wa wasichana wa shule wapatao 200 kutoka mji wa
Chibok kaskazini mashariki mwa Nigeria mwezi Aprili mwaka 2014, uliibua hasira
ya kimataifa.
Kundi hilo limeungana na kundi la Daesh linalofanya
harakati zake za uasi katika nchi za Syria na Iraq.

0 comments:
Post a Comment