![]() |
| Watu wapatao 50 wamefariki dunia katika mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Ethiopia. |
Kwa uchache watu 50 wamepoteza maisha katika mafuriko na
maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Ethiopia.
Kiasi cha watu 41 wamefariki dunia katika mkoa wa Wolayita
kusini mwa taifa hilo kutokana na maporomoko ya ardhi, vyombo vya habari nchini
humi vimemnukuu afisa wa polisi wa eneo hilo, Alemayehu Mamo.
Ripoti zinasema kuwa watu wengine tisa wamepoteza maisha
katika mkoa wa Bale kusini mwa nchi hiyo kufuatia mafuriko makubwa. Zaidi ya ng’ombe
1,000 wameripotiwa kuzama katika eneo hilo.
Makumi kwa maelfu ya watu wameathiriwa na mvua kubwa
katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Barabara kadhaa zimeharibiwa na madaraja
kusombwa na maji.
Nchi hiyo imekuwa katika changamoto kubwa ya ukame mbaya
kabisa ambao umeikumba kwa miongo mingi, lakini mvua kubwa zisizotabirika
zimesababisha uharibifu katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Ukame ulioikumba Ethiopia na baadhi ya mataifa ya Afrika
umeongezewa na hali mbaya na ya muda mrefu ya El Nino iliyodumu kwa miaka 35,
na kusababisha ukame wa mvua kati Oktoba na Desmba mwaka jana tangu mwaka 1981.
El Nino imesababishwa joto kubwa na ukame katika mataifa
ya kusini mwa Afrika kama vile Malawi, Afrika Kusini, Zimbabwe, Lesotho,
Angola, Mozambique, Namibia na Zambia.
Hali hiyo imesababishwa baadhi ya maeneo duniani kuwa na
joto kali na kusababisha mvua kubwa katika maeneo mengine.
Kupata habari kupitia WhatsApp: +255 712 566 595
Kupata habari kupitia WhatsApp: +255 712 566 595

0 comments:
Post a Comment