Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohmaed Shein anatarajiwa kuzindua Baraza jipya la Wawakilishi Machi 30 ikiwa ni hatua za kuelekea kuanza kazi za Serikali baada ya kumalizika uchaguzi mkuu.
Akizungumza na wandishi wa habari Katibu wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Yahaya Khamis Hamad akiongea na waandishi wa habari amesema
kwamujibu wa Katiba na taratibu za kuendesha Baraza la Wawakilishi Rais
wa Zanzibar ndiye mweye mamlaka ya kuitisha kikao hicho ambapo pia
amesema watakitumia kuwaapisha Wajumbe wa Baraza na kuteua Wajumbe
watano watakaowakilisha Baraza ndani ya Bunge.
Mapema Mtendaji huyo wa Baraza alimkabidhi fomu ya kugombea uspika
kwa mgombea wa CCM Zubeir Ali Maulid huku akithibitisha kuwa ni mgombea
pekee aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo,ambapo akiongea na waandishi
mgombea Uspika ambaye ni wa CCM na ana uhakika wa kupata kiti hicho
amesisitiza ahadi zake kuwa Baraza pamoja kuwa ni la CCM halitoyumba na
litakuwa na meno.
Baraza hilo la Wawakilishi limekamilika baada ya Uchaguzi Mkuu
ambapo Majimbo 54 yamechukuliwa na CCM na viti 22 ni viti maalum vya
wanawake huku Mjumbe mwingine na Mwanasheria Mkuu Wazanzibar huku kukiwa
kumebakia nafasi10 za upendeleo za Rais ambapo litafanya baraza hilo
kuwa na wajumbe 88 pamoja na spika.

0 comments:
Post a Comment