Wanachama 89 wa
kundi la Kiislamu la Boko Haram nchini Nigeria wamehukumiwa kifo nchini
Cameroon baada ya kupatikana na makosa kujihusisha na ugaidi.
Eneo hilo limekuwa likishambuliwa mara kwa mara na wanamgambo wa Boko Haram.
Waliohukumiwa ni sehemu ya wanachama 850 wanaozuiliwa nchini Cameroon kwa kudaiwa kuhusika na mashambulio ya kundi hilo la Kiislamu.
Hii ni mara ya kwanza kwa watu kuhukumiwa kifo chini ya sheria mpya za kukabiliana na ugaidi zilizopitishwa mwaka 2014.
Sheria hiyo hupendekeza kifo kwa wanaopatikana na makosa ya ugaidi.
Watu 22 walihukumiwa kifo mwaka 2013.
BBC

0 comments:
Post a Comment