
Ndege moja ya shirika la ndege la Egypt Air inayofanya
safari za ndani kutokea Alexandria kwenda
Cairo imetekwa na kupelekwa katika uwanja wa ndege wa Larnaca nchini Cyprus,
redio ya serikali imesema.
Shirika la Utangazaji la Cyprus (CBC) limesema kuwa
ndege hiyo aina ya Airbus 320 ilikuwa na watu 55 wakiwemo wafanyakazi saba.
Polisi ya Cyprus ilisema kuwa mtekaji huyo aliwasiliana
na chumba cha kuongozea ndege na kuruhusiwa kutua.
Inaripotiwa kuwa mtekaji huyo alimtisha rubani akisema
kuwa amevaa mkanda wenye milipuko. Shirika la ndege la Egypt Air limesema kuwa
mtekaji aliwaachia watu wote waliokuwa kwenye ndege isipokuwa abiria watatu na
wafanyakazi wanne.
Shirika la habari la serikali, MENA, limesema kuwa
mtekaji huyo ni raia wa Misri aitwaye Ibrahim Samaha. Alikuwa amekaa kwenye
kiti namba K38, imesema bila kutoa maelezo ya kina.

Shirika la habari la Cyprus limesma kuwa nchini humo kuna
mwanamke aliyekuwa mke wa zamani wa mtu huyo na kwamba anaweza kuwa na sababu
binafsi za kufanya tukio hilo.
Mashuhuda wanasema kuwa mtu huyo alirusha barua kwenye
aproni ya uwanja wa ndege iliyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, akitaka ifikishwe
kwa mkewe huyo wa zamani kwenye asili ya Cyprus.
Uwanja wa ndege wa Larnaca umefungwa na magari ya
wagonjwa yametumwa kwenye eneo la tukio.
0 comments:
Post a Comment