ACT-Wazalendo Haishiriki uchaguzi Zanzibar
TAARIFA KWA UMMA:
Tumekuwa tukipokea simu za waandishi mbali mbali
baada ya kauli ya jana ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),Jecha
Salum Jecha kuwa hakuna chama kilichojitoa katika uchaguzi unaotarajiwa
kufanyika machi 20 mwaka huu
Msimamo wa ACT-Wazalendo ni kuwa hatutashiriki
Uchaguzi huo kama ilivyoazimiwa katika kikao cha kamati kuu cha february 14
mwaka huu
Hatushiriki kwa kuwa tunaamini kuwa hakuna sababu ya
kufanyika uchaguzi mwingine nje ya ule uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana
Taarifa hii ya kutoshiriki uchaguzi wa machi 20
mwaka huu imewasilishwa katika ofisi ya ZEC Zanzibar february 9 mwaka huu baada
ya wao kututaka tuthibitishe kwa maandishi kama tutashiriki au la
Hivyo kauli ya Jecha kuwa hakuna chama kilichofuata
utaratibu ni muendelezo mwingine wa kutaka kuhalalisha haramu kuwa halali kama
walivyofanya katika kufuta uchaguzi wa Oktoba 25
Kwa kuthibitisha dhamira yetu hii ya kutoshiriki
hivi karibuni kamati Maalum ya uongozi Zanzibar ilimsimamisha uanachama ndugu
Khamis Idi Lila,aliyedhaminiwa na chama kuwania nafasi ya urais wa Zanzibar
katika uchaguzi uliofutwa kwa "Zengwe" hivyo hatuna mwanachama
anayewania nafasi hiyo
Jecha amezungumzia Sheria ya Uchaguzi na wajibu wa
mgombea aliyedhaminiwa na chama kuthibitisha ushiriki wake,huku akiacha kwa
makusudi kuainisha udhamini huo ni katika uchaguzi gani
ACT-Wazalendo haijamdhamini mwanachama wake yeyote
kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Machi 20 na hili lilipewa msisitizo katika
kikao cha kamati kuu iliyofanyika february 14 na taarifa kutolewa kwa umma siku
iliyofuata
Tunaomba wananchi wapuuze ulazimishaji huu wa ZEC
kwa kutaka kuionesha dunia kuwa vyama vimeshiriki uchaguzi huo haramu
ACT wazalendo katika kikao chake cha kamati kuu
iliazimia kuwa haitakuwa muhuri wa kuwasafisha wabakaji wa Demokrasia kwa
kushiriki uchaguzi wa Machi 20
Abdallah Khamis
Afisa Habari
ACT Wazalendo
22/2/2016
0 comments:
Post a Comment