
Kukithiri kwa
biashara haramu ya ngono pamoja na tabia ya ushoga mkoani Iringa kunadaiwa
kusababishwa na baadhi ya vijana wa vyuo vikuu wanafika mkoani humo kwa ajili
ya masomo ya elimu ya juu, huku miongoni mwao wakitaka starehe zilizo nje ya
uwezo wao.
Tamaa ya kumiliki vitu vya thamani – ni miongoni mwa
mambo yanayotajwa kuwahadaa baadhi ya
wasomi hao wa vyuo vikuu, jambo linalosababisha wengi wao kuangukia katika
wimbi la biashara ya ngono na ushoga na kuufanya ongezeko la maambukzi ya vvu.
Kwa mkoa wa iringa inadaiwa kuwa zaidi ya mashoga 1500
wamejitangaza wenyewe kuendesha biashara
haramu ya ngono, jambo ambalo kiafya linadaiwa kuwa ni hatari kwa maambukizi ya virus vya ukimwi.
Baadhi ya
wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani iringa
ndiyo wanaonyooshewa kidole kuhusika na biashara hiyo ya ngono na tabia ya
ushoga- ambapo shirika la restless development linalojihusisha na masuala ya
afya ya uzazi na makuzi kwa vijana- kupitia mradi wa dance for life-
limewakutanisha viongozi hawa wa serikali ya wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani
iringa- ili kujadili namna ya kujinasua
katika wimbi hilo la ushoga na biashara haramu ya ngono.
Serikali inaona
tatizo hilo la ushoga na biashara ya ngono litamalizwa na jamii yenyewe,
endapo tu wazazi na walezi watakemea
mapema mienendo hatarishi ya vijana wao.
Ushoga ni tabia inayofanywa na baadhi ya wanaume,
kwa kujihusisha kimapenzi na wanaume
wenzao, suala ambalo kwa kiwango kikubwa
linatajwa kuchochewa na mambo ya utandawazi, ambao unaibua mitindo mbalimbali
na tabia mpya kila uchwao.
0 comments:
Post a Comment