
Polisi katika jimbo la Edo nchini Nogeria wameripotiwa
kumtia nguvuni kasisi mmoja wa kanisa la kiinjili mchungaji Ikenna Okafor na
wamepanga kumfungulia mashitaka kwa tuhuma za kuzika hirizi katika viwanja vya
kanisa lake katika mji wa Benin.
Ingawa kilichozikwa na mtuhumiwa hakijawekwa wazi na
polisi, inashukiwa kuwa ni mabaki ya viungo vya mnyama fulani. Matumizi ya
hirizi ni jambo la kawaida sana nchini Nigeria, hata makanisani, ambapo
taratibu za ibada za kimila huchanganywa na taratibu za kidini na baadhi ya
makasisi hutumia hirizi ili kuponya baadhi ya magonjwa.
Katika tukio hili, wakazi wanaoishi jirani na kanisa
hilo lililopo katika Mtaa wa Esigie katika mji wa Benin walidai kuwa ilikuwa ni
myama fulani aliye hai. Baada ya kumkamata mchungaji Okafor, polisi walimtoa
eneo hilo ili kumuepusha asipigwe na wakazi wenye hasira waliovamia viwanja
hivyo.
Shuhuda mmoja aitwaye Chinedu Nnamdi, alisema kuwa baba
yake alimuamsha saa 8 usiku siku ya Jumamosi kushuhudiwa kilichokuwa kikifanywa
na mchungaji huyo. Aliongeza kuwa alimuona mchungaji akizika kitu mbele ya
kanisa na baadae kufanya taratibu fulani kwa kulizunguka jengo la kanisa mara
kadhaa.
Naibu mrakibu wa Polisi, Osifo Abiodun, ambaye ni
msemaji wa jeshi hilo katika jimbo la Edo, amesema kuwa mshukiwa yuko chini ya
upelelezi. Alifafanua kuwa mchungaji huyo alitoa maelezo muhimu yatakayosaidia
jeshi hilo katika upelelezi wao.
CHANZO: Nigerian Watch
0 comments:
Post a Comment