![]() |
| Sultan Hassanal Bolkiah wa Brunei |
Nchi ya Somalia yenye idadi kubwa ya Waislamu imepiga
marufuku sherehe za Christmas baada nchi ya Brunei ya kusini mashariki mwa Asia
kuchukua hatua kama hiyo mapema mwezi huu na kutoa onyo la kifungo cha miaka
mitano jela kwa yeyote atakayekiuka agizo hilo.
Mapema siku ya Jumanne Sheikh Mohamed Khayrow, mkurugezi
mkuu katika wizara ya masuala ya dini, alisema kuwa sherehe za Christmas na
Mwaka Mpya ni kinyume na mafundisho ya imani ya Kiislamu.
"Hakutakuwa na sherehe zozote hata kidogo," aliwaambia
wanahabari, na kuongeza kuwa vikosi vya usalama vimeagizwa kuchukua hatua dhidi
ya atakayekiuka agizo hilo.
"Matukio yote yanayohusiana na Christmas na Mwaka
Mpya yanapingana na utamaduni wa Kiislamu, na yanaweza kuwa na taathira mbaya
kwa jamii ya Kiislamu.”
Naye Sheikh Nur Barud Gurhan, kutoka Baraza Kuu la
Waislamu nchini humo, alionya dhidi ya sherehe hizo, akisema kuwa zinaweza
kuwahamasisha al-Shabab "kufanya mashambulizi".
Mwaka jana kundi hilo lilifanya mashambulizi siku ya Christmas
dhidi ya makao ya vikosi vya Umoja wa Afrika yenye ulinzi mkali katika mji mkuu
Mogadishu, na kuua askari watatu na raia mmoja.
Somalia, ambayo ilipiga marufuku kama hiyo mwaka 2013, inafuata
kalenda ya Kiislamu ambayo haitambui Januari 1 kama mwanzo wa mwaka.
Wanadiplomasia kutoka nje, wafanyakazi wa mashirika ya
misaada, na askari wanaoishi katika makao ya vikosi vya Umoja wa Afrika
wanaruhusiwa kusherehekea siku hiyo kwa namna binafsi, sio hadharani.
KOFIA ZA SANTA ZAPIGWA MARUFUKU
Wakati Somalia ikichukua hatua hizo, sultani wa Brunei, Hassanal
Bolkiah amechukua hatua kama hiyo kwa kupiga marufuku maadhimisho ya Christmas
hadharani.
Viongozi wa kidini katika taifa hilo lenye utajiri wa
mafuta walitahadharisha kuwa sherehe za Christmas zitapigwa marufuku kwa nguvu
zote, huku wale watakaokiuka wakikabiliwa na kifungo cha mpaka miaka mitano
jela.
"Matumizi ya alama za kidini kama vile misalaba,
kuwasha mishumaa, kutengeneza miti ya Christmas, nyimbo za kidini, kutuma
salamu za Christmas… ni kinyume na mafundisho ya imani ya Kiislamu,” maimamu
walisema katika taarifa iliyochapishwa na vyombo vya habari nchini humo.
Mwaka jana serikali ilionya kwamba Waislamu watakuwa
wanafanya kosa kubwa kuvaa “kofia au mavazi ya Santa Claus".
Wakristo nchini humo ni asilimia 9 tu ya raia wa taifa
hilo wapatao 430,000.
CHANZO: Aljazeera

0 comments:
Post a Comment