![]() |
Rais wa FIFA Joseph Sepp Blatter (kushoto) akizungumza
na Rais wa UEFA Michel François Platini wakati wa mkutano wa 64 wa FIFA uliofanyika
mjini Sao Paulo, nchini Brazil, Juni 11, 2014.
|
Shiriko la Soka Duniani (FIFA) limempiga marufuku rais
wake, Joseph Sepp Blatter, na rais wa muungano wa vyama vya soka barani Ulaya (UEFA),
Michel François Platini, kutojihusisha na shughuli za soka kwa miaka minane.
Kamati ya maadili ya Shirikisho hilo limewakuta wawili
hao na hatia ya kutumia vibaya nafasi zao kufuatia malipo ya kitita kipatacho milioni
mbili za franca za Uswizi (zaidi ya dola milioni mbili) kilichotolewa na
Blatter mwaka 2011 kwenda kwa Platini.
Aidha, Blatter amepigwa faini ya franca 50,000 za Uswizi
($50,250), wakati Platini akipigwa faini
ya franca 80,000 ($80,400).
“Katika maelezo yake ya maandishi wala katika maelezo yam
domo, bwana Blatter hakuweza kuonesha kuonesha msingi mwingine wa kisheria wa
malipo haya. Kwa kushindwa kuweka mbele maslahi ya FIFA na kuacha kufanya jambo
lolote ambalo linapingana na maslahi ya FIFA, Bwana Blatter alikiuka jukumu
lake la kimaadili kwa FIFA,” walisema majaji.
Waliongeza kuwa, “Mada yake (Blatter) kuhusu makubaliano
ya mdomo yalionekana kuwa hayana nguvu na kukataliwa na jopo.”
Aidha, majaji hao walisema kuwa Platini “alishindwa kutenda
kulingana na uaminifu na uadilifu, na kuonesha kutojua umuhimu wa majukumu yake.”
Uamuzi wa jopo hilo la maadili lililoongozwa na Hans
Joachim Eckert, umehitimisha vuta ni kuvute ya Blatter na Platini juu ya soka
la kimataifa na kuondosha ndoto zao za kugombea urais wa FIFA katika uchaguzi
utakaofanyika Februari 26 mwaka ujao.

0 comments:
Post a Comment