
Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Barcelona, Chelsea,
Inter Milan na Everton ameteuliwa kuwa kocha wa klabu ya Antalyaspor ya nchini
Uturuki, baada ya kuondoka kwa kocha mkuu Yusuf Simsek. Mkongwe huyo wa Cameroon
aliyejiunga na klabu hiyo mwezi Juni kwa mkataba wa miaka mitatu, alitaarifiwa
na rais wa klabu hiyo kuchukua majukumu ya ukufunzi pamoja na mkurugezi wa
ufundi Mehmet Ugurlu mpaka kocha mpya atakapoajiriwa.
"Tulikaa na [mkurugenzi wa ufundi] Mehmet Ugurlu na
Eto'o. wote wawili wataungana katika mafunzo. Bodi imewapa Ugurlu na Eto'o jukumu
la mafunzo mpaka kocha mpya atakapopatikana,” rais wa klabu, Gultekin Gencer aliliambia
shirika la habari la DHA.
Kwa jukumu hilo jipya, sasa Eto'o atakuwa na majukumu
mawili ya ukocha na kuwa mchezaji. Kwa sasa Eto’o ndiye mfungaji wa bora wa Super
Lig akiwa na magoli 13 katika mechi zake 15 za mwanzo na Antalyaspor. Klabu imempa
mshambuliaji huyo mechi tatu za kujithmini, kisha atathmini upya hali baada ya
mapumziko ya ligi hiyo.
Mwaka 2005, Eto’o alishika nafasi ya tatu katika uteuzi
wa FIFA wa mchezaji bora wa mwaka, na amewahi kuteuliwa mara nne kuwa mchezaji
bora wa Afrika. Alishinda makombe mawili ya Michuano ya Mataifa ya Afrika, na
ndiye mshindi wa taji la mfungaji bora wa michuano hiyo.
Mfungaji bora huyo wa timu ya taifa ya Cameroon,
alishiriki katika makombe manne ya dunia, na makombe sita ya michuano ya
mataifa ya Afrika.
0 comments:
Post a Comment