
Shule na vyuo binafsi vitakabiliwa na upungufu mkubwa wa
walimu kuanzia mwaka ujao wa masomo kufuatia walimu wengi wa kigeni kuondoka
nchini kutokana na kukosa vibali vya kazi.
Uondokaji wa walimu hao ni pigo kubwa kwa shule binafsi
ambazo zinategemea sana walimu wa kigeni.
Chama cha Waendeshaji na Wamiliki wa Shule na Vyuo
visivyokuwa vya kiserikali (Tamongsco) jana kilielezea wasiwasi huo na kusema
kuwa kwa uchache walimu 3,400 wameshaondoka nchini.
“Kutokana na uondokaji huu, ndani ya wiki mbili zijazo
shule hazitakuwa na walimu wa kigeni,” katibu mkuu wa Tamongsco, Benjamin
Nkonya, aliiambia the The Citizen jana jijini Dar es Salaam.
Hilo limetokea kufuatia agizo la serikali linalowataka
waajiri wote kuhakikisha waajiriwa wao wasiokuwa raia wanafanya kazi kihalali
kwa kuwapatia vibali vya kazi badala nyaraka za muda (CTA).
Katika tangazo hilo, serikali imetoa muda wa mpaka
mwishoni mwa mwezi huu kwa waajiri kufuata sheria ya ajira kwa raia wa kigeni
kwa kuhakikisha wanawapatia vibali vya kazi wafanyakazi wao.
Kwa sasa, gharama ya kibali cha kazi ni dola 2,500 (takriban
milioni 5) ambayo, kwa mujibi wa bwana Nkonya, shule hizo haziwezi kumudu.
Ingawa hakuzitaja shule ambazo zimeathirika, alisema
kuwa nyingi ni za mikoa ya Dar es Salaam, Kilimanjaro, na Kagera. Wageni wanaofanya
kazi katika shule binafsi nchini wengi wao wanatoka katika nchi za Kenya,
Uganda, Malawi, na Rwanda.
Akielezea suala hilo, katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Prof Sifuni Mchome, amesema kuwa suala hilo liko chini ya
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hata hivyo, alisema ingawa nchi ilikuwa na upungufu wa
walimu wa sayansi, mchakato wa kuwaajiri wa kigeni ulipaswa kufuatwa, wakati Tamongsco
ikiendelea kuishawishi serikali kuondoa ada ya vibali vya kazi.
Katibu mkuu huyo alibainisha kuwa nchi inakabiliwa na
upungufu wa walimu 27,000 wa masomo ya sayansi, na kwamba lilikuwa jambo jema
kuwaajiri kutoka nje ya nchi.
Prof Mchome alisema kuwa Tamongsco ilijaribu, bila
mafanikio, kufuatilia ombi lake la kuitaka serikali iondoa ada ya vibali vya
kazi ambayo iliwekwa kwa walimu wa kigeni.
CHANZO: The Citizen
0 comments:
Post a Comment