![]() |
| Picha iliyopigwa Oktoba 23, 215 mjini Mauduguri, kaskazini mwa Nigeria, ikiwaonesha watu wakiwa wamesimama msikitini baada ya mlipuko wa bomu. |
Watu ishirini wameuawa na wengine 90 kujeruhiwa katika
mlipuko uliotokea kwenye msikiti mmoja kaskazini mwa Nigeria.
Kwa mujibu wa Wakala wa Usimamizi wa Matukio ya Dharura
nchini humo (NEMA), mlipuko huo umetokea katika msikiti katika mji mkuu wa
jimbo la Borno kaskazini mwa nchi hiyo, siku moja baada ya wapiganaji wa Boko
Haram kushambulia eneo la Jiddari Polo kwenye viunga vya mji wa Maiduguri, shambulizi
lililosababisha vifo vya watu 15.
Mlipuko huo umetokea katika eneo ambalo siku ya Jumapili
jeshi la nchi hiyo lilijibizana risasi na kundi hilo baada ya kupanga kufanya
mashambulizi katika mji wa Maiduguri.
"Jana sote tulikimbia baada ya nyumba zetu kushika
moto. Asubuhi tumerudi, na wakati tukihesabu idadi ya watu walioungua ndani ya
nyumba hizo, bomu lingine likalipuka,” alisema Ibrahim Goni, mkaazi
aliyetembelea eneo la mlipuko huo.
Hakuna kundi au mtu ambaye amedai kuhusika na mlipuko
huo, lakini mara nyingi maafisa wa Nigeria wamekuwa wakilitupia lawama kundi la
Boko Haram kwa matukio hayo, kundi ambalo limekuwa likidaiwa kufanya mashambulizi
makali tangu mwaka 2009.
Raisa wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari, amevipa vikosi vya
nchi hiyo muda wa hadi mwishoni mwa mwaka huu kuliangamiza kundi hilo.
Uasi wa kundi hilo umeripotwa kupoteza maisha ya watu 20,000
na wengine zaidi ya 2.5 kupoteza makazi tangu mwaka 2009.
The group has expanded its attacks to neighboring
African countries including Chad, Niger and Cameroon.

0 comments:
Post a Comment