![]() |
Dkt John Magufuli akiongea na wafanyabiashara kwenye
mkutano uliofanyika Alhamis hii ikulu jijini Dar es Salaam (Picha: Michuzi)
|
Mkutano wa leo kati ya Rais Dkt John Magufuli na
wafanyabiashara nchini kwenye ikulu ya Dar es Salaam haukuwa wa kunywa chai na
cocktail bali wenye maelekezo muhimu na mazito.
Katika mkutano huo, Magufuli ametoa siku saba, kuanzia
leo kwa wafanyabiashara wote walioingiza bidhaa nchini bila kulipa ushuru
wakajisalimishe na kulipa.
Mkutano huo umehudhuriwa na wawakilishi wa Tanzania
Private Sector Foundation wakiongozwa na Mwenyekiti Dk. Reginald Mengi, CEOs
Round Table wakiongozwa na Mwenyekiti, Ali Mfuruki na baraza la biashara Taifa,
TNBC.
Hatua hiyo imekuja kufuatia hatua kali zilizoanza
kuchukuliwa dhidi ya ukwepaji kodi unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa.
Hivi karibuni Magufuli alimsimamisha kazi kamishna mkuu
wa TRA, Rished Bade kufuatia kupotea kwa makontena zaidi ya 300 kwenye bandari
ya Dar es Salaam.

0 comments:
Post a Comment