Zahran Alloush, mkuu wa kundi la Jaysh al-Islam, ambalo
ni miongoni mwa makundi ya waasi yenye nguvu sana katika viunga vya mji wa Damascus
vinavyoshikiliwa na waasi, ameuawa katika shambulizi la ndege lililoyalenga
makao makuu ya kundi hilo, duru za jeshi la Syria na waasi zimesema.
Duru mbili za waasi zimesema kuwa makao ya siri ya kundi
hilo, ambalo ndio kundi kubwa kabisa katika eneo hilo na lenye maelfu ya
wapiganaji, yalilengwa na kile walichosema kuwa ni ndege za Urusi.
Jeshi la Syria limesema kuwa Zahran Alloush aliuawa katika
shambulio la ndege dhidi ya ngome yake katike eneo la Ghouta ya Mashariki
kwenye viunga vya mashariki vya mji mkuu.
Viongozi kadhaa wa makundi ya waasi wameripotiwa kuuawa
tangu Urusi ilipoanza mashambulizi makubwa ya anga Septemba 30 katika kumuunga
mkono mshirika wake Rais Bashar al-Assad, ambaye vikosi vyake mwaka huu
vilionekana kuzidiwa.
Kundi la Jaysh al-Islam, lenye maelfu ya wapiganaji
waliopewa mafunzo, ndio kundi kubwa na linaloonekana kujipanga vizuri. Limekuwa
likitawala katika eneo la Kusini mwa Ghouta.
Wakati huo huo, kundi hilo limemtangazaAbu Hammam Bowydany kuwa mrithi wa Zahran atakayeliongza kundi hilo.
Kabla ya kuanzisha kundi la Jaysh al-Islam, Alloush alikuwa
ameanzisha kundi la Liwa al-Islam, au Brigedi ya Uislamu, kwa kushirikiana na
baba yake Abdallah, anayedaiwa kuishi nchini Saudi Arabia.
Alloush alikuwa katika mgogoro wa kimsingi na makundi ya
Dola ya Kiislamu katika Iraq na Sham (ISIS) na al-Qaeda, kwa kuonekana kuwa mtu
mwenye nadharia za msimamo wa wastani wa Uislamu.
CHANZO: Today’s zaman na mashirika ya habari.

0 comments:
Post a Comment