![]() |
| Rais Dk John Magufuli |
Rais John Magufuli leo anatarajiwa kukutana na jumuiya
ya wafanyabiashara jijini Dar es Salaam katika kile kinachoonekana kama hatua
za makusudi za Mkuu huyo wa Nchi kuelezea mipango na matarajio yake kwa sekta
binafsi wakati wa utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni.
Japokuwa kikao hicho ni cha kawaida kwenye kalenda ya
Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) – ambacho huongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania – Dkt Magufuli anaonekana kuwa na ujumbe madhubuti wa
namna utawala wake unavyotaka kuwa na ushirikiano na sekta binafsi.
Hayo yanafanyika kwa sababu kikao hicho kimekuja chini
ya mwezi mmoja tangu alipoapishwa na kabla hajaunda baraza lake la mawaziri.
Aidha, yanafanyika takriban mwezi mmoja tangu mtangulizi
wake, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, aongoze kikao kama hicho Oktoba 2.
Taarifa iliyotolewa na katibu mtendaji wa TNBC, Bwana
Raymond Mbilinyi, imesema kuwa Rais atatumia mkutano huo kuzunguza na kujadili
na wafanyabiashara ili kuwa na diria ya pamoja katika kufikia maendeleo
yanayotarajiwa.
Na, iwapo hali itakuwa hivyo, inatarajiwa kuwa Dkt
Magufuli atawaasa wafanyabiashara kuchukua hatua za makusudi za kulipa kodi
badala ya kufshirikiana na watumishi wasio waaminifu katika kukwepa kodi.
Ijumaa iliyopita, Rais Magufuli na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, walimsimamisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na
maafisa waandamizi watano baada ya kuagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa
kiasi cha shilingi bilioni 80 zilizotakiwa kulipwa kodi.
Mpaka sasa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Athumani
Diwani, ameripoti kwamba watu wapatao 12 wamekamatwa kuhusiana na skendo hiyo.
Hilo linaonekana kama utekelezaji wa kile ambacho Dk
Magufuli alikisema wakati wa hotuba yake ya kulizindua Bunge mjini Dodoma wiki
mbili zilizopita alipoashiria kwamba serikali yake haitamvumilia afisa yeyote
wa TRA atakayekuwa kikwazo cha serikali kukusanya kodi, hususan kutoka kwa
wafanyabiashara wakubwa.
Wakati wa hotuba yake hiyo, Dk Magufuli aliorodhesha
ofisadi kama tatizo la kwanza alililokumbana nalo wakati wa kampeni za
uchaguzi.
Alieleza pia kuwa anataka kuona ufisadi, rushwa na
urasimu vikizikwa na kuwa historia.
Ni kwa sababu hiyo kwamba Dk Magufuli atatoa onyo kwa
watumishi wa umma kuhusu suala la urasimu ambalo limekuwa changamoto kubwa
katika ufanyaji biashara nchini kiasi kwamba baadhi ya wawekezaji huamua kwenda
nchi nyingine kuwekeza.
CHANZO: The Citizen

0 comments:
Post a Comment