
Uturuki imepeleka vifaru vya ziada, magari ya kijeshi na
silaha nyingine kwenye mpaka wake na Syria leo Jumamosi baada ya tukio la jeshi
lake kuiangusha ndege ya kijeshi ya Urusi lililoongeza joto na mivutano baina
ya nchi hizo mbili.
Msafara wa vifaa na zana hizo za kivita kutoka mikoa ya
magharibi uliingia katika mkoa wa mpakani wa Gaziantep.
Siku moja kabla, msafara mwingine wa vifaru ulipelekwa
kwenye mpaka wa Uturuki na Syria.
Mapema Jumanne, ndege mbele za Uturuki aina ya F-16 zikiwa
katika doria ziliigundua ndege ya kivita iliyokuwa ikiingia katika anga ya
Uturuki kwenye mpaka wa nchi hiyo na Syria na baada ya kuionya mara 10 ziliamua
kudungua.
Baadae Wizara ya Ulinzi ya Urusi ilitangaza kuwa ndege
yake aina ya SU-24 ilikuwa imetunguliwa. Ilianguka katika mkoa wa Syria wa Bayirbucak
karibu na wilaya ya Yayladagi ya mkoa wa Hatay kusini mwa Uturuki.
0 comments:
Post a Comment