![]() |
| Ndege ya Urusi aina ya Sukhoi Su-24 ikiruka kutoka uwanja wa Humeimim katika mkoa wa Latakia nchini Syria. |
Ndege ya kivita ya Urusi imetunguliwa leo na jeshi la
anga la Uturuki katika mkoa wa Kızıldağ karibu na mpaka wa Syria.
Ikulu ya Uturuki imethibitisha kuwa ndege hiyi aina ya SU-24
imetunguliwa baada ya kuingia katika anga ya nchi hiyo.
Taarifa iiliyotolewa na jeshi la anga la nchi hiyo
imesema kuwa ndege hiyo ilionywa mara 10 ndani ya dakika 5 kabla ya
kutunguliwa.
Marubani wawili wameripotiwa kuruka kwa kutumia miamvuli
yao. Haijawa wazi iwapo wamepona au la.
Hata hivyo, Urusi imekanusha kuwa ndege yake ilikiuka sheria
za anga, na taarifa ya wazara ya ulinzi imeeleza kuwa helkopta za Urusi
zinafanya uchunguzi katika eneo hilo katika juhudi za kuwatafuta marubani wake.

0 comments:
Post a Comment