![]() |
| Rais wa Urusi Vladmir Putin |
Rias wa Urusi Vladimir Putin amechaguliwa na jarida la
Forbes kwa mara ya tatu kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani.
Putin amempita Rais wa Marekani Barack Obama, ambaye
amekuwa wa tatu baada ya Kansela wa Ugerumani Angela Merkel, aliyechaguliwa
kuwa mwanamke mwenye nguvu na ushawishi mkubwa zaidi duniani katika orodha hiyo
ya saba inayotolewa kila mwaka na iliyochapishwa jana Jumatano.
"Putin ameendelea kuthibitisha kwamba yeye ni
miongoni mwa watu wachache duniani wenye uwezo wa kufanya kile wanachokitaka,”
limeandika jarida hilo.
Kwa mujibu wa makala hayo, ushawishi wa Putin ndani ya
nchi yake umepanda mpaka asilimia 89, ambacho ni kiwango cha juu zaidi ndani ya
miaka sita.
USHAWISHI WA OBAMA UMETIKISIKA
Obama amekuwa rais wa
kwanza wa Marekani aliye madarakani aliyeshindwa kuwa katika mbili bora. "Wakati
Obama akiwa katika mwaka wa mwisho wa utawala wake, ni wazi kuwa ushawishi wake
umetikisika, na imekuwa ngumu zaidi kufanikisha mambo,” limesema jarida hilo.
Kati ya watu 73 katika
orodha hiyo ya mwaka 2015, Papa Francis amekuwa wa nne huku Rais wa China Xi
Jinping akishika nafasi ya tano, ambapo ameporomoka kwa nafasi mbili za mwaka
jana.

0 comments:
Post a Comment