ANTALYA, Uturuki
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa
mashambulizi ya Ijumaa mjini Paris yameonesha kwamba uchumi na usalama wa dunia
ni mambo yenye uhusiano, na kuongeza kuwa masuala ya kiulimwengu kama vile
ugaidi, vita vya kiraia nchini Syria na tatizo la wakimbizi ni mambo
yanayohitaji juhudi za dunia nzima.
"Mashambulizi
ya kigaidi mjini Paris kwa mara nyingine yameonesha kuwa kuna uhusiano mkubwa
baina ya uchumi na usalama na hatuwezi kuupuuza uhusiano huu wa karibu”,
amesema Erdogan wakati wa ufunguzi wa mkutano wa viongozi wa mataifa 20 yenye
uchumi mkubwa duniani (G20) unaofanyika katika mji wa Antalya kusini mwa
Uturuki.
Rais huyo amesema kuwa suala la uchumi ndio lengo kuu la
G20 lakini jukwaa hilo la kimataifa haliwezi kukwepa jukumu la kushughulikia
matatizo ya kisiasa, kijamii au kiutamaduni yanayoisumbua dunia.
"Matukio yote haya yanatuonesha kuwa ugaidi ni
tishio kwa amani na usalama wetu sote. Sisi kama Uturuki, tunaamini kwamba ushirikiano
imara baina ya mataifa katika kukabiliana na ugaidi ni jambo ambalo tunapaswa
kulichukulia azma madhubuti.”
Kuhusu kadhia ya wakimbizi, Erdogan aliashiria wazi kuwa
jumuiya ya kimataifa “imeshindwa mtihani huo”.
Erdogan amesema kuwa wakati Uturuki ikikalia kiti cha
uongozi wa G20, imefanya maamuzi makubwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na miundombinu, nishati na kuongeza fursa za ajira kwa wanawake.
"[G20] sio sio taasisi tutakayoikumbuka kama jukwaa
wakati wa matatizo pekee. Bali kuna matarajio mengine ambayo dunia inayatarajia
kutoka kwetu. Kwa kulielewa hili, ningependa kusema kuwa uenyekiti wa Uturuki
umejikita kwenye ushirikishaji, utekelezaji na uwekezaji. Katika utamaduni na
ustaarabu wetu, haya ndio mambo muhimu.”
"Dhana ya haki ni dhana nyeti katika utamaduni
wetu. Ninaamini kwamba inaafikiana na ushirikishaji katika majukumu ya G20. Jambo
hilo tumelipa umhimu wa karibu. Kipaumbele cha pili ni utekelezaji: hakika
tunataka kutekeleza kauli na ahadi zetu. Jambo la tatu ni uwekezaji. Takribani katika
mataifa yote yaliyoendelea na yanayoendelea bado kuna hitajio la miundombinu. Kwa
muktadha huu wanachama wetu wanatilia maanani vipaumbele hivi kwa ajili ya
maslahi ya nchi zao. Wameweka mikakati ya uwekezaji ambayo wataitekeleza,”
amesema Erdogan.
Uturuki ni mwenyeji wa mkutano wa 10 viongozi wa mataifa
20 yenye uchumi mkubwa (G20), ambao unajadili matatizo makubwa ya kisiasa na
kiusalama duniani ikiwemo suala la Syria na tatizo la wakimbizi.
CHANZO: Anadolu Agency
0 comments:
Post a Comment