![]() |
| Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda. |
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, kwa mara
nyingine tena imeahirisha hukumu ya kesi ya jinai inayomkabili Kiongozi wa
Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini Sheikh Ponda Issa Ponda.
Kesi hiyo iliyotarajiwa kutolewa hukumu yake leo
Jumatano na Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Mary Moyo imeahirishwa na mshtakiwa
amerudishwa rumande baada ya hakimu husika kutokuwepo mahakamani hapo kwa madai
kuwa amekwenda kwenye kozi fupi ya kushughulikia kesi za uchaguzi mjini
Dodoma ambapo shauri hilo limelazimika kuahirishwa na
Hakimu Mkazi, Erick Rwehumbiza hadi Novemba 30, mwaka huu itakapofikishwa tena
mahakamani hapo.
Mshtakiwa huyo anakabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo
kutoa maneno yenye kuhimiza imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa,
mashtaka anayodaiwa kuyatenda Agosti 2013.
Upande wa mashtaka wa kesi hiyo unawakilishwa Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Benard Kongola, Sunday Hyera na George Mbalasa, wakati
upande wa Mshitakiwa unawakilishwa na Wakili Juma Nasoro, Abubakar Salim na
Bartholomeo Tarimo.
Awali hukumu ya Sheikh Ponda ilipangwa kutolewa 19, 10
kabla ya kuahirishwa tena na shauri hilo kupangwa kutolewa hukumu Novemba 18
mwaka huu, kabla ya kuahirishwa tena hii leo hadi Novemba 30.

0 comments:
Post a Comment