![]() |
| Brigedia Jenerali Farshad Hassounizadeh aliyeuawa Oktoba 12, 2015 nchini Syria. |
Majenerani wawili wa Kiiran wameuawa nchini Syria katika
mapambano na wanamgambo wa kundi la Dola
ya Kiislamu katika Iraq na Sham (ISIS), ripoti zinasema.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Hamid
Mokhtarband na Farshad Hassounizadeh, ambao wote wana cheo cha brigedia
jenerali katika jeshi la walinzi wa mapinduzi la nchi hiyo, wameuawa jana
Jumatatu.
![]() |
| Brigedia Jenerali Hamid Mokhtarband aliyeuawa nchini Syria mnamo Oktoba 12, 2015 |
Majerali hao wameuawa siku chache baada ya kuuawa kwa
kamanda mwandamizi katika jeshi hilo, Brigedia Jenerali Hossein Hamedani,
ambaye aliuawa na wanamgambo hao katika viunga vya mji wa Aleppo kaskazini mwa
Syria.
Iran ilituma askari kumsaidia rais wa nchi ya Syria,
Bashar Al-Assad, anayepambana na uasi uliodumu kwa muda wa miaka 4 sasa.
Ghasia nchini humo zilizuka mwezi Machi 2001 na mpaka
sasa zaidi ya watu 250,000 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya milioni moja
wamejeruhiwa, kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa.


0 comments:
Post a Comment