Ripoti zinasema kuwa kwa uchache watu 65 wamepoteza
maisha baada ya winchi kuwaangukia Mahujaji katika Msikiti Mkuu wa Makka, Saudi
Arabia.
Mamlaka ya nchi hiyo zimethibitisha kutokea kwa tukio
hilo, na kueleza kuwa zaidi ya watu 154 wamejeruhiwa.
Duru kutoka nchini humo zinasema kuwa upepo mkali
ulioandamana na kimbunga ndio uliosababisha kuanguka kwa winchi hiyo.
Mashuhuda wanasema kuwa magari ya wagonjwa yaliwasili
katika eneo hilo na kuwaondoa majeruhi.
Miradi kadhaa ya ujenzi imekuwa ikifanyika katika mji wa
Makka kwa miaka kadhaa. Miradi hiyo inalenga kuupanua Msikiti Mkuu na maeneo
yanayouzunguka.





0 comments:
Post a Comment