![]() |
| Rais wa Guatemala Otto Perez Molina |
RAIS wa Guatemala, Otto Perez Molina, amejiuzulu muda
mfupi baada ya kutolewa kibali cha kukamatwa kufuatia skendo ya ufisadi
ulioitikisa serikali yake.
Kiongozi huyo ameamua kung’atuka madarakani ili
kupambana yeye mwenyewe dhidi ya mashitaka yanayomkabili, amesema msemaji wake Jorge
Ortega.
Kung’atuka huko kumekuja saa chache baada ya jaji kutoa
kibali cha kukamatwa wakati mashitaka yakiandaliwa dhidi ya tuhuma za ufisadi
zinazodaiwa kufanywa na utawala wake.
Kutokana na amri hiyo ya mahakama, Perez Molina atalazimika
kufika mbele ya jaji Miguel Angel Galvea kujibu mashitaka ya matumizi mabaya ya
madaraka, ukwepaji kodi na upokeaji rushwa.
Mapema juzi Jumanne, Bunge la nchi hiyo lilimuondolea
kinga ya kutoshitakiwa na hivyo kuandaa mazingira ya kushitakiwa kwa tuhuma za
kuhusika na mpango wa kifisadi ambao wafanyabiashara wanaripotiwa kuwa walitoa
hongo ili kukwepa ushuru wa forodha.
Perez Molina mwenye umri wa miaka 64, amekanusha tuhuma
hizo na kuahidi kukabiliana na mkondo wa sheria. Mpaka sasa hakuna mashitaka
yaliyowasilishwa dhidi yake.
Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo kwa
rais aliye madarakani kufikishwa mbele ya sheria.
Viongozi wa wafanyabiashara, Baraza la Maaskofu wa nchi
hiyo na hata ofisi ya mdhibiti wa mahesabu ya serikali walikuwa wamemtaka Perez
Molina kujiuzulu.
Soma zaidi kuhusu skendo hiyo>>>http://www.mzizima24.com/2015/09/guatemala-yamzuia-rais-kusafiri-nje-ya.html
Soma zaidi kuhusu skendo hiyo>>>http://www.mzizima24.com/2015/09/guatemala-yamzuia-rais-kusafiri-nje-ya.html

0 comments:
Post a Comment