
Katika mchezo wa kuvutia dhidi ya Espanyol hapo jana, Cristiano
Ronaldo alifunga mabao 5 – ikiwa ni pamoja na hat trick – na kuweka rikodi mpya
kama mchezaji wa Real Madrid aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya
ligi kuu ya Hispania maarufu kama La Liga.
Nyota huyo kutoka Ureno ameifungua Real Madrid mabao 230
katika La Liga, mabao mawili zaidi ya Raul Gonzales aliyekuwa akishikilia
rekodi hiyo.
Mshindi huyo wa Ballon d'Or wa mwaka 2015 alitumia
michezo 204 kufunga mabao mawili zaidi ya Raul aliyetumikia michezo 550.
Jana Real Madrid iliichachafanya Espanyol 6 – 0 (Benzema
28, Cristiano Ronaldo, 7, 17 (P), 20, 62 na 81) katika mchezo wa ugenini na
hivyo kushikilia uongozi wa ligi kwa muda baada ya michezo mitatu.
Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo kufunga magoli 5 katika
mechi moja, mara ya kwanza ikiwa ni katika mchezo dhidi ya Granada mwezi Aprili
(9 – 1).
Orodha ya wafungaji bora katika La Liga inaongozwa na Lionel
Messi (286), akifuatiwa na Hugo Sanchez (234), Telmo Zarra (251) na Cristiano
Ronaldo.
Ronaldo alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Manchester
United kwa kitita cha uhamisho wa yuro milioni 94 kilichovunja rekodi wakati
huo.
0 comments:
Post a Comment