
“Sera ya kumwaga tshs 50m kwa kila kijiji ni moja ya
sera za kutawanya ufisadi nchini. Wakati hatujui mabilioni ya JK yaliishia wapi
na hata taarifa ya CAG kuhusu fedha hizi kufichwa zinakuja hizi za kugawa hovyo
hovyo. Mpango huu unapaswa kupingwa na kila Mtanzania. Tanzania ina zaidi ya
vijiji 12,000 na hivyo fedha zitakazorushwarushwa hovyo ni tshs 600 bilioni.
Zitatoka wapi? Tukatae ubabaishaji huu kwenye uchumi wa nchi yetu. Watanzania
wanataka Hifadhi ya Jamii ili wapate Afya bure na mafao mengine.”
0 comments:
Post a Comment