
Mlipuko katika soko moja katika jimbo la Borno kaskazini
mashariki mwa Nigeria umewaua watu wasiopungua 47 na kuwajeruhi wengine 52.
Duru za kijeshi na kiusalama zimesema kuwa mlipuko huo
umetokea katika mji wa Sabon Gari.
Wiki chache zilizopita mji huo ulishuhudia mamia ya watu
wakipoteza maisha katika mashambulizi yanayohusishwa na kundi la Boko Haram.
0 comments:
Post a Comment