
Musoma. Mama mmoja amechanganyikiwa baada ya mwanaye wa
siku moja kuibiwa na mtu asiyejulikana katika Hospitali ya Rufaa mkoani Mara.
Mama huyo, Msuba Elias,17, alisema kuwa kwenye majira ya
saa 2 asubuhi mwanamke mmoja alikwenda moja kwa moja kwenye kitanda chake na
kumuuliza jina lake. Kisha alimwambia kuwa nesi katika wodi namba nane alikuwa
akimuita.
Baada ya kufika kwa nesi aliyedaiwa kumuita, alikataa. Alirudi
wodini lakini alishtuka baada ya mwanaye kutokuwa kitandani. Alimuuliza mama
mwingine aliyekuwa amelala kwenye kitanda cha jirani akamwambia kuwa mwanaye
alichukuliwa na mtoto mmoja.
Alimtafuta mwanaye katika maeneo mbalimbali hospitalini
hapo bila mafanikio, ndipo aliposhauriwa kuliripoti suala hilo katika kituo
kikuu cha polisi mjini Musoma.
Kwa mujibu wa Bi. Musiba, alibeba ujauzito alipokuwa
kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Iyovu wilayani Bukombe, mkoani
Geita.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mara Philip Kalangi amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa ya kina itatolewa baadaye kwa
waandishi wa habari.
CHANZO: The Citizen
0 comments:
Post a Comment