
Wakazi wa kijiji cha Bundo katika Kaunti ya Nyamira nchini
Kenya bado wapo katika hali ya utata mkubwa baada ya shughuli moja ya mazishi
kusitishwa kufuatia tukio la mchanga ‘kufufuka’.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Citizen Digital, baba
wa mtoto huyo anasema kuwa siku ya Jumapili mkewe aliyekuwa na ujauzito wa
miezi saba alijifungua mtoto ambaye hajakomaa na baadaye kupelekwa katika
hospitali ya Nyamira kwa matibabu.
Aliongeza kuwa mtoto huyo aliwekwa katika chumba cha
watoto mpaka jana Jumanne ambapo wauguzi wa hospitali hiyo walitangaza kuwa
mtoto huyo amekufa, jambo lililopelekea familia kuandaa taratibu za mazishi.
Mambo yalibadilika baada ya mwanamke mmoja kuomba auone
mwili wa mtoto huyo ili atoe heshima zake za mwisho lakini akashtuka kuona ‘maiti’
ikitabasamu ndani ya jeneza.
Mama wa mtoto huyo ambaye alishtushwa na taarifa hizo na
ambaye bado yuko hospitali, alielezea furaha yake baada ya kuambiwa kuwa
mwanaye bado yu hai.
CHANZO: Citizen Digital
0 comments:
Post a Comment