Mama mmoja nchini Malaysia, Madam Meliah Diah, anakadiriwa
kuwa na umri wa miaka 101 na anaweza kuonekana kuwa mtu aliyedhoofika sana,
lakini hilo halimzuii kumtunza na kumhudumia mwanaye mlemavu mwenye umri wa
miaka 63, Abdul Rahman Saud.
Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Harian Metro, mjane
huyo ambaye kwa sasa anaonekana kama ishara na nembo ya upendo wa mama,
ameendelea kumlea mwanaye huyo akiwa peke yake baada ya mumewe kufariki dunia
miaka 22 iliyopita.
Anamlisha, kumuogesha, kumsafisha na kumuweka juani kila
siku.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa kuwa kila siku asubuhi, Madam
Meliah humuogesha kwenye varanda la nyumba yao ya miti katika kijiji cha Bukit
Nambua, katika mji wa Kedah. Akimaliza kumuogesha humlisha na kukaa hapo kwa
siku nzima kabla ya kumrudisha ndani wakati wa jioni.
Diah amuambia mtandao wa Metro:
"Matatizo ya kifafa yaliyomkumba akiwa
mdogo yamemfanya awe hivi. Muda wote anakuwa amelala kifudifudi na kusogea
kidogo kidogo.
Anapenda kula wali. Tuko peke yetu, hatuna
mtu mwingine. Ninatumai kuwa nisifariki dunia kabla yake kwa sababu hakuna mtu
atakayemhudumia na kumtunza.”
0 comments:
Post a Comment