WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anapewa nafasi
kubwa ya kupitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea wake wa nafasi ya
urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Raia Mwema limeambiwa.
Mchakato wa kutafuta mgombea ndani ya CCM unatarajiwa
kuhitimishwa Jumapili wiki hii mjini Dodoma, wakati Mkutano Mkuu wa chama hicho
utakapokaa kuchagua mrithi wa Rais Jakaya Kikwete.
Duru za kisiasa ndani ya CCM na serikalini zinaonyesha
kuwa Magufuli ndiye anayepewa nafasi zaidi; huku kwa sababu tofauti, majina ya
Bernard Membe na Jaji Augustino Ramadhani yakitajwa kama watu wanaomkaribia.
“Ni Magufuli. Ni bahati mbaya tu kwamba waandishi wa
habari na wachambuzi wa kisiasa hamjui kufuatilia siasa kwa karibu.
Hamjajiuliza tu kwa nini yeye hajamponda mwenzake yeyote wala serikali kwenye
kusaka wadhamini?
“Kuna waziri gani kwenye serikali ya Kikwete anayeweza
kusema ni mtekelezaji mkubwa wa ilani ya uchaguzi ya CCM kuliko Magufuli na
wananchi wakamwelewa? Angetaka angejitapa lakini aliamua kukaa kimya na hii ni
kwa sababu anajua anachofanya.
“Hajajinadi kwa sababu anajua chama kitamnadi wakati
utakapofika na yeye mwenyewe ni mzungumzaji mzuri kama akiamua. Amejitahidi
sana ‘kutocheza rafu’ ili asionekane kuvunja kanuni na taratibu za chama.
“Amejishusha sana na hii si kawaida. Hajatangaza nia kwa
mbwembwe kama wengine na anajua Watanzania wanampenda na kumfahamu. Ukifanya
calculations zako utaona kwamba yeye ndiye aliyeandaliwa,” kilisema chanzo cha
kuaminika cha gazeti hili kutoka CCM.
Tofauti na mawaziri wengine na watu wanaoonekana mbele
yake kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais, Magufuli alitafuta wadhamini wake
kimyakimya na mara chache alisikika akizungumza.
Wakati wagombea wengine walitumia muda mrefu kueleza
upungufu uliopo ndani ya chama na serikali na namna watakavyobadilisha mambo
endapo watapata nafasi, Magufuli hakuahidi chochote na badala yake akasema
atafuata ilani ya chama.
Kauli hiyo ya Magufuli ilifanana na ile iliyotolewa na
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula, aliyesema kwamba chama ndicho
kinachopaswa kuwanadi wagombea na si wagombea wenyewe kujinadi.
Gazeti hili lilikuwa la kwanza kutoa taarifa rasmi
kwamba Magufuli atajitosa kuwania urais; likinukuu chanzo kutoka nchini Kenya
ambako waziri huyo alikwenda kwenye msiba wa mtoto wa swahiba wake wa kisiasa,
Raila Odinga, Fidel.
Baadaye, Magufuli alizungumza na gazeti dada la hili,
Raia Tanzania na kuthibitisha kwamba atachukua fomu za kuwania urais, mara
baada ya kipyenga kupulizwa ndani ya CCM.
Alipoulizwa endapo atawania urais, Magufuli alijibu;
“Swali hili nimeulizwa mara nyingi. Mara zote nimekataa kulijibu kwa sababu
chama chetu (CCM) kuna utaratibu wake wa namna ya kuomba nafasi ya uongozi.
Muda ulikuwa haujawadia.
“Lakini utakumbuka wiki hii hapa hapa Dodoma, vikao vya
juu vya chama chetu vimetoa ratiba kwa wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali
kujitokeza.
“Kwa maana hiyo sasa niko huru kujibu swali lako kwa
kusema rasmi ‘nitagombea urais’. Nafanya hivyo kwa sababu naamini ninazo sifa
za kuchagua na kuchaguliwa kama mwanachama wa CCM kwa nafasi yoyote
inayojitokeza kulingana na Katiba ya chama chetu na pia Katiba ya nchi,”
alisema Dk. Magufuli.
Kwenye kuwania kwake urais, Magufuli alitangaza kupitia
gazeti hilo pekee.
KWA NINI MAGUFULI
Magufuli ni mmoja wa wanasiasa nchini ambao
wamejipambanua kama wachapakazi –sifa inayoonekana kuwa adimu miongoni mwa kada
ya watawala waliopo sasa.
Umaarufu wake uliibuka wakati wa utawala wa Rais
Benjamin Mkapa na alifahamika kwa umahiri wa kukariri kumbukumbu mbalimbali za
ujenzi wa barabara uliokuwa ukifanywa wakati wa Mkapa.
Raia Mwema limeambiwa kwamba kutokana na madai kuwa Rais
Kikwete hakuwa mfuatiliaji mzuri kwenye utawala wake, nchi inahitaji Rais
atakayekuwa mfuatiliaji na mtendaji zaidi na Magufuli anaonekana kufaa kwenye
eneo hilo.
Magufuli ana kete ya kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa hapa nchini ambayo kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ndiyo itakayokuwa na wapiga kura wengi miongoni mwa kanda nyingine hapa nchini. Makadrio ya NEC ni wapiga kura milioni 24 nchi nzima kwa mwaka huu.

Wapanga mikakati ndani ya CCM wanaamini kuwa kama
Magufuli atapata mgombea mwenza mwanamke endapo atapitishwa, chama kitakuwa
kimeua ndege wawili kwa jiwe moja; kura kutoka eneo lenye watu wengi na za
wanawake ambao wana matamanio ya kumwona mmoja wao kwenye mojawapo ya nafasi za
juu.
Wakati Raia Mwema likiandika habari za Magufuli kwa mara
ya kwanza, lilikuwa limeambiwa na vyanzo vyake kuwa Rais Kikwete alikuwa
akifurahi kusafiri mikoani na waziri wake huyo kwa sababu wafuasi wa vyama vya
upinzani hawakuwa wakizomea wakati Magufuli akizungumza.
Tukio lililofungua macho ya Kikwete linadaiwa kutokea
mkoani Mwanza wakati mawaziri wengine walipokuwa wakizomewa huku wakijieleza
lakini aliposimama Magufuli, wananchi walimshangilia ingawa eneo hilo
lilidaiwa, kwa wakati huo, kuwa ngome ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Mmoja wa mawaziri wa CCM walio karibu na Magufuli alifananisha kupitishwa kwa Magufuli na ilivyokuwa mwaka 1995 wakati Mkapa alipopitishwa ingawa hakuwa mgombea mwenye nguvu ndani ya chama.
Mmoja wa mawaziri wa CCM walio karibu na Magufuli alifananisha kupitishwa kwa Magufuli na ilivyokuwa mwaka 1995 wakati Mkapa alipopitishwa ingawa hakuwa mgombea mwenye nguvu ndani ya chama.
“Kuhusu Magufuli, simuoni kama mtu mwenye nguvu ndani ya
chama. Kwenye chama chetu kuna wanachama wa aina mbili; kuna wale tunaowaita
Native CCM (CCM asilia) na Migrant CCM (Wahamiaji).
“Magufuli ni migrant. Hawa ni wale ambao wametumika
zaidi serikalini kuliko kwenye chama. Hana ushawishi mkubwa miongoni mwa
wajumbe wa NEC wala Mkutano Mkuu. Lakini usisahau, hata Benjamin Mkapa naye
hakuwa asilia. Alikuwa mhamiaji lakini akawashinda wale asilia.
“Namna pekee ya wahamiaji kushinda ni endapo CCM itaamua
kuwa na mgombea wa namna hiyo na hilo linawezekana kwa sababu limewahi kutokea
huko nyuma.
“Huu ni uchaguzi ambao ajenda kubwa itakuwa ni
uwajibikaji na ufisadi. Ni nani anaweza kupeperusha vizuri bendera ya CCM
kwenye eneo hilo kama si yeye? CCM itakuwa inaonyesha picha gani kwa kumpitisha
mtu ambaye uwajibikaji wake una walakini?” alisema waziri huyo ambaye hatutamtaja
jina kwa sasa kwa sababu maoni yake hayapaswi kuwekwa hadharani kutokana na
nafasi yake ndani ya chama.
JAJI
RAMADHANI
Raia Mwema limeambiwa pia kuwa kuna uwezekano wa CCM
kumpitisha Jaji Mkuu mstaafu, Augustino Ramadhani, kuwa mgombea wake ili atumike
kwa kipindi cha mpito cha miaka mitano.
Gazeti hili linafahamu kuwa kutokana na mchakato wa
kutafuta Katiba Mpya ambao umeanza tayari, kuna watu ndani ya CCM wanaoona kuwa
anahitajika Rais atakayesimamia mchakato huo hadi mwisho na muda huohuo
ukatumika kukijenga upya chama.
Jaji huyo alikuwa amestaafu Ujaji Mkuu na Raia Mwema
linafahamu kuwa alikataa kuongeza muda wake wa kustaafu (ambao unaruhusiwa
kisheria) wakati alipoombwa kwa vile alitaka kufanya kazi ya kumtumikia Mungu
kanisani.
Akiwa tayari mchungaji katika Kanisa la Anglikana na kila mtu akiamini kuwa maisha yake ya utumishi wa umma yamemalizika, jina lake likaibuliwa ghafla katika kinyang’anyiro.
Akiwa tayari mchungaji katika Kanisa la Anglikana na kila mtu akiamini kuwa maisha yake ya utumishi wa umma yamemalizika, jina lake likaibuliwa ghafla katika kinyang’anyiro.
Ana sifa ya kuwa Mzanzibari ambaye uchaguzi wake unaweza
kuimarisha Muungano na kuondoa manung’uniko kuwa upande huo wa Muungano
haujapewa nafasi tangu Ali Hassan Mwinyi.
Kama ilivyo kwa Magufuli, naye hana kashfa yoyote ya rushwa na hivyo anaweza kusimamia masuala ya uwajibikaji na uadilifu pasipo shaka yoyote.
Kuna wanaoamini kuwa kuchaguliwa kwake kutalipooza kundi la wazee wa chama hicho, kama akina Jaji Joseph Warioba na Joseph Butiku, ambao hawakufurahishwa na namna serikali ilivyolishughulikia suala la Katiba ambapo Jaji Ramadhani alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Raia Mwema limeambiwa kwamba endapo Jaji Ramadhani atapitishwa, Dk. Asha Rose Migiro au mmoja wa wanaotaka urais sasa kupitia CCM kutoka mojawapo ya kambi zenye nguvu Tanzania Bara, anaweza kupitishwa kuwa mgombea mwenza.

Jaji Augustino anapewa nafasi pia kwa sababu wengi
wanaona ni lazima kuna makubaliano maalumu yaliyopo yaliyomfanya akubali
kupumzika Uchungaji na kuingia kwenye siasa.
Julai 12 mwaka huu, itafahamika ni nini kilichomfanya
aingie kwenye siasa.
BERNARD MEMBE
Jina la Waziri huyu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa nalo linatajwa kwa sababu ana sifa zinazofanana na alizokuwa nazo
Mkapa na anaelezwa kuwa na ushawishi kwenye jumuiya ya kimataifa.
Magufuli na Ramadhani hawana ushawishi sana kwenye siasa za kimataifa kama alivyo Membe ambaye amekuwa waziri wa wizara hiyo kwa muda wa miaka minane.
Magufuli na Ramadhani hawana ushawishi sana kwenye siasa za kimataifa kama alivyo Membe ambaye amekuwa waziri wa wizara hiyo kwa muda wa miaka minane.
Marais wawili waliopita waliomtangulia Membe –Kikwete na
Mkapa, waliwahi kuwa mawaziri wa mambo ya nje kabla hawajawa marais na kutokana
na mahitaji ya dunia ya sasa ya kitandawazi, jina lake linaendelea kutajwa kama
chaguo namba tatu.
Membe pia hana tuhuma za ufisadi zinazomzinga na jambo hilo ni kete katika uchaguzi wa mwaka huu.
Membe pia hana tuhuma za ufisadi zinazomzinga na jambo hilo ni kete katika uchaguzi wa mwaka huu.
WAJUMBE WA MKUTANO MKUU
Mkutano Mkuu wa CCM utakaokutana Jumamosi na Jumapili
ijayo ulitakiwa kuwa na wajumbe halali 2,422 lakini wajumbe 14 hawapo kwa
sababu mbalimbali zikiwamo vifo, ugonjwa na sababu nyingine na hivyo Raia Mwema
linafahamu waliothibitisha kwenda Dodoma hadi juzi Jumatatu ni 2,408.
Mshindi ambaye ndiye atakuwa mgombea wa CCM anapaswa kupata zaidi ya nusu ya kura zote za wajumbe na hivyo namba 1,205 ndiyo itakuwa namba ya maajabu.
Mshindi ambaye ndiye atakuwa mgombea wa CCM anapaswa kupata zaidi ya nusu ya kura zote za wajumbe na hivyo namba 1,205 ndiyo itakuwa namba ya maajabu.
Safari hii mkutano huo utafanyika katika ukumbi mpya wa
CCM ujulikanao kwa jina la Dodoma Convention Centre (DCC) uliopo nje kidogo ya
mji huo.
Safari hii, kama jogoo atawika (alivyokuwa akiimba hayati Kapteni John Komba) basi hatawika kutoka Chimwaga bali itakuwa kutoka DCC.
Safari hii, kama jogoo atawika (alivyokuwa akiimba hayati Kapteni John Komba) basi hatawika kutoka Chimwaga bali itakuwa kutoka DCC.
CHANZO: Raia Mwema
0 comments:
Post a Comment