1. Mchakato wa uteuzi: Yaonekana kuwa vyama vinavyounda
umoja huo viliingia katika mchakato wa uteuzi bila makubaliano thabiti juu ya
namna watakavyomteua mgombe wao wa kiti cha urais.
2. Majimbo: Kuna utata pia kuhusu kugawana majimbo,
ambapo chama cha NCCR-Mageuzi kinalalamika kuwa kimepewa majimbo machache sana.
3. Ilani ya Uchaguzi: Haijawa wazi ni ilani ipi ambayo
mgombea wa Ukawa ataitumia. Yaonekana kuwa jambo hili litaibua mashaka miongoni
mwa vyama husika kutokana na kila chama kuwa na mipango yake ya namna kitakavyofanya
pindi kikichaguliwa.
4. Kutoaminiana: Kuna hali ya kutoaminiana na kutiliana
shaka miongoni mwa wajumbe wa Ukawa huku kukiwa na hisia kwamba Chadema, ambacho
ndio chama kikubwa, kinatumia umoja huo kwa maslahi yake binafsi.
0 comments:
Post a Comment