
Viongozi wa ACT Wazalendo safarini Ujerumani kwa mwaliko
wa chama cha Die Linke
Mwenyekiti wa chama cha act wazalendo mama Anna Mghwira
akiongozana na katibu mkuu Ndugu samson mwigamba na katibu wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa ndugu Venance Msebo leo tarehe 15 julai 2015 wameanza
ziara ya siku saba nchini ujerumani kwa mwaliko wa chama rafiki cha kijamaa
(Die Linke Party).
Katika ziara hiyo pamoja na kutembelea die linke party,
watapata fursa ya kutembelea ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani na pia
watafanya mkutano na watanzania wanaoishi nchini ujerumani katika kuwahamasisha
kuchangia maendeleo ya nchi yao na pia kutafuta fursa kurudi nyumbani
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kupiga kura
ifikapo Oktoba mwaka huu.
Imetolewa na afisa habari,
Act wazalendo
Abdallah Khamis
15 julai 2015
0 comments:
Post a Comment