![]() |
| Riek Machar |
Kiongozi wa waasi Sudan Kusini Riek Machar ametishia
kuandaa mapinduzi dhidi ya Rais Salva Kiir iwapo atakaa kuondoka madarakani
mpaka kufikia usiku wa leo.
Machar amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi nchini
Kenya kuwa mhumula wa utawala wa Kiir unafikia tamati usiku wa leo na kumtaka
ajiuzulu kwa heshima ili kupisha mchakato wa uchaguzi.
Anautuhumu utawala wa Rais Kiir kwa kujaribu kufanya
mabadiliko ya katiba ili kujiongezea muhula wa kukaa madarakani isivyo halali.
Akizungumza na mkutano huo wa wanahabari, Machar alionya
kuwa iwapo Kiir hataondoka madarakani, wananchi wa Sudan Kusini watakuwa na
kila haki ya kufanya uasi na kuuondosha kwa nguvu utawala wake.
Ametoa vitisho hivyo katika kilele cha maadhimisho ya 4
ya uhuru wa taifa hilo kutoka Jamhuri ya Sudan.

0 comments:
Post a Comment