HAMAD WA CUF AJIUNGA RASMI ADC

Outgoing Wawi MP Hamad Rashid Mohamed (right)
Aliyekuwa mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohammed (kulia) akikabidhiwa kadi mpya ya uanachama wa chama cha ADC kutoka kwa mwenyekiti wa chama hicho Said Miraj Abdullah jijini Dar es Salaam jana.


Dar es Salaam. Ni rasmi sasa kwamba Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohammed ni mwanachama wa chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) baada ya jana kukabidhiwa kadi namba 1 ya chama hicho kufuatia kesi yake na chama chake cha zamani cha Civic United Front (CUF) kufutwa.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa chama hicho, Said Miraaj, kadi hiyo ilitunzwa kwa ajili yake kwa kuwa ni miongoni mwa wanachama waasisi wa chama hicho kilichoanzishwa mwaka 2012 baada ya Bwana Mohammed kufukuzwa katika chama cha CUF pamoja na wanachama wengine kadhaa.

Mwaka jana, ADC ilitangaza kuwa Bwana Mohammed ana nia ya kugombea kiti cha Urais kupitia chama hicho lakini kesi yake na CUF ilizuia jambo hilo mpaka juzi Jumatano kesi hiyo ilipofutwa na mahakama.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo, Bwana Mohammed alisema kuwa hana uadui na chama chake cha zamani na aliahidi kushirikiana na vyama vingine ili kudumisha amani na utulivu nchini.

“Kwa kuwa bila amani maendeleo hayawezi kupatikana, nimejiunga ADC kwa sababu ninaamini ni chama kinachosimamia ustawi wa wananchi kwanza,” alisema.

Katika hotuba yake, mwenyekiti wa chama Bwana Miraaj alisema kuwa ADC iko tayari kuungana na vyama vingine vinavyoweka mbele maslahi ya wananchi.

“Milango yetu iko wazi, lakini tungependa muungano ambao sio wa kugombania majimbo, vyeo au ruzuku. Tuko tayari kuzitoa mhanga nyadhifa zetu iwapo tutaungana kwa ajili ya wananchi,” alisema bwana Miraaj.

Mapema mwenyekiti huyo alitumia hotuba yake kuiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufikiria kuongeza muda wa uandikishaji wa wapiga kura katika jiji la Dar es Salaam kufuatia kuibuka kwa matatizo yanayochelewesha mchakato huo.

Kwa upande mwingine, naibu katibu mkuu wa chama hicho, Doyo Hassan, alielezea wasiwasi wake juu ya kadi bandia za kupigia kura akisema kuwa kukosekana kwa taarifa muhimu ya tarehe ya usajili itapelekea watu wengine kubuni vitambulisho bandia.

“Nina kitambulisho changu hapa lakini hakioneshi tarehe ya kuandikishwa, hili linaibua wasiwasi ya vitambulisho bandia kutumika wakati wa upigaji kura. Ninashangaa kwa nini NEC haikuweka taarifa hii muhimu kama ilivyofanya kwa vitambulisho vya zamani,” alihoji.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment