![]() |
Wahudumu wa huduma za dharura wakimuingiza muathirika
katika gari ya wagonjwa kufuatia mlipuko wa bomu kwenye kituo kimoja cha polisi
katika mkoa wa kaskazini wa Al-Arish Aprili 12, 2015.
|
Kwa uchache askari 60 wa Misri wameuawa na wengine
kadhaa kujeruhiwa katika mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo kwenye
vizuizi vya kijeshi katika eneo la Peninsula ya Sinai linaloendelea kushuhudia
mawimbi ya ghasia.
Duru za kijeshi zinasema kuwa wapiganaji hao walilipua
gari lililojazwa milipuko kusini mwa mji wa Sheikh Zuweid, kilometa 334 (maili 214)
kaskazini mashariki mwa mji mkuu, Cairo, leo Jumatano, na kuwaua makumi ya
askari huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.
Kwa mujibu wa televisheni ya Sky News Arabia,
washambuliaji hao pia walifanya mashambulizi kwenye vizuizi vya kijeshi katika
wilaya za al-Joureh, Abu Refaei na Sedrah kwenye viunga vya kusini vya mji wa Sheikh
Zuweid.
Milipuko hiyo ilifuatia ufyatulianaji wa risasi baina ya
vikosi vya serikali ya Misri na wapiganaji hao.
Wakati huo huo, waasi waiopungua 10 wameuawa na wengine
kadhaa kujeruhiwa baada ya helkopta za jeshi la Misri kushambulia maficho yao
katika Peninsula ya Sinai.
Hatua hiyo inakuja zikiwa zimepita siku kadhaa baada ya
waasi wasiopungua 11 kuuawa na wengine kukamatwa wakati askari wa serikali
walipoyashambulia maficho ya wanamgambo hao katika mji wa Sheikh Zuweid na
katika mji wa mpakani wa Rafah, kilometa 340 (maili 211) mashariki mwa Cairo.
![]() |
Picha ya maktaba ikiwaonesha wanamgambo wa kundi la Wilayat
Sinai, ambao zamani walijulikana kama Ansar Bait al-Maqdis, katika eneo la Peninsula ya Sinai.
|
Jeshi la Misri linaliona eneo la Peninsula ya Sinai kuwa
kichaka cha wanamgambo.
Wanamgambo hao wamezidisha mashambulizi tangu Mohamed
Morsi, rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, alipopinduliwa na jeshi mnamo
Julai 2013.
Wanamgambo kutoka kundi la Wilayat Sinai, ambao zamani
walijulikana kama Ansar Bait al-Maqdis, wamedai kuhusika na mashambulizi mengi
katika Peninsula ya Sinai.


0 comments:
Post a Comment