waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano 2015/16

TAARIFA KWA UMMA

OWM-TAMISEMI inawatangazia majina ya wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2015.
Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Jumla ya wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na wavulana
31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana 11,450 na
wavulana 18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansi
na Hisabati; na wanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 na
wavulana 13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomo
ya Sanaa na Biashara.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015
wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai, 2015 na hakutakuwa na
fursa ya mabadiliko yoyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa
kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi
atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya
kuripoti, nafasi yake itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa
nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na
Vyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatikana kwenye tovuti ya OWMTAMISEMI
ya www.pmoralg.go.tz

Imetolewa na Katibu Mkuu,


Download Hapa
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment