![]() |
Nyumba zilizoharibiwa vibaya na maporomoko ya ardhi
katika mji wa Darejeeling, nchini India, Julai 1, 2015.
|
Kwa uchache watu 21 wamepoteza maisha katika maporomoko
ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa katika jimbo la Bengal nchini India.
Kwa mujibu wa polisi, kadhia hiyo imeiathiri miji ya Mirik,
Kalimpong, na Darjeeling.
Aidha, imeripotiwa kuwa zaidi ya nyumba 100 na barabara
vimeharibiwa vibaya katika miji hiyo.
Kadhia hii inatokea wiki moja baada ya watu wasiopungua
55 kupoteza maisha katika mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliyolikumba jimbo
la Gujarat magharibi mwa India.
Mafuriko la maporomoko ya ardhi ni matukio yanayolikumba
eneo la Asia ya Kusini kila mwaka katika msimu kama huu.

0 comments:
Post a Comment