
Askari kutoka kikosi cha Umoja wa Afrika (AU) nchini
Somalia, AMISOM, wamekosolewa kufuatia mfululizo wa vifo vya raia nchini
Somalia.
Vyombo vya habari
na wahudumu wa afya nchini humo wanawatuhuma askari wa AU kwa kuua raia
wasiopungua 22 ambao wamedai kuwa hawakuwa na silaha.
Tukio hilo linadaiwa kutokea katika mji wa Marka, kusini
mwa Somalia.
Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Al Jazeera, askari wa
AU waliwafyatulia risasi vijana wasiokuwa na silaha waliokuwa wakicheza mpira.
Wakazi kadhaa walikimbia kuepuka mzozo huo. AMISOM imekanusha
vikali madai hayo na kuweka ujumbe kwenye mtandao wa Twitter unaokanusha
kutokea kwa tukio hilo.
Katika taarifa yake iliyotolewa Julai 21, 2015, AMISOM
imesema kuwa askari wake walikutana na wapiganaji wa Al Shabaab na kuwaua
wapiganaji watano.
Zaidi ya askari 20,000 kutoka mataifa kadhaa ya Afrika
wanaunda kikosi cha AMISOM. Kikosi hicho kinapambana na wanamgambo wa Al
Shabaab nchini Somalia.
0 comments:
Post a Comment