ATEKETEZA FAMILIA YA MCHUMBA WAKE KWA MGOGORO WA MAHARI


Mourners gather around the dead bodies of their relatives in the northern Pakistani city of Peshawar on April 5, 2015. (AFP PHOTO)
Waombolezaji wakiwa pembezoni mwa miili ya ndugu zao waliouawa katika mji wa Peshawar kaskazini mwa Pakistan Aprili 5, 2105.

Mwanaume mmoja nchini Pakistani awaua watu 10 akiwemo mchumba wake kutokana na kutoelewana mahari.

Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Polisi ni kwamba mwanaume huyo baada ya kuwaua wazazi wake na ndugu zake wawili miezi 6 iliyopita kwa kukataa kumtolea mahari, alivamia nyumba moja usiku na kuwafyatulia risasi watu 10 katika familia moja walipokuwa wamelala akiwemo mchumba wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kamanda wa Polisi katika mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akitafutwa na polisi tangu alipowaua wazazi wake miezi 6 iliyopita.

Kijana huyo alitumia bunduki aina ya AK-47 katika shambulio alilotekeleza katika kitongoji cha Charsadda.

Kijana huyo anaishi mafichoni tangu alipowaua wazazi wake mwaka 2014 baada ya kukataa kumtolea mahari kiwanja cha familia kilichokuwa kimeombwa na mzazi wa mchumba wake.


Polisi imeeleza kuwa huenda M.Khan alitekeleza shambulio hilo dhidi ya wakwe zake kutokana na mahari ya thamani kubwa waliyokuwa wameomba.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment