Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mheshimiwa
Bernard Membe (kushoto), aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, akiungana na (kutoka
kushoto) Rais Paul Kagame wa Rwanda, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na marais Uhuru
Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Salva Kiir wa Sudan Kusini wakiwashuhudia
Waziri wa fedha wa Kenya Henry Rotich na
Waziri wa Biashara wa China Gao Hucheng wakisaini makubaliano ya ujenzi wa reli
ya kisasa itakayoziunganisha Mombasa na Malaba kwenye mpaka wa Kenya na Uganda.
Shughuli hiyo ilifanyika jana katika Ikulu ya Kenya mjini Nairobi.
MAKUBALIANO rasmi ya mipango ya ujenzi wa njia mpya ya
reli Afrika Mashariki kwa msaada wa China umesainiwa katika mji mkuu wa Kenya,
Nairobi.
Reli hiyo inatarajiwa kuanzia Mombasa mpaka Nairobi na
kisha kuelekea katika nchi za Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.
Reli hiyo ikuwa mbadala wa ile ya zamani iliyojengwa na
utawala wa kikoloni zaidi ya miaka 100
iliyopita.
China itafadhili asilimia 90 ya gharama ya awamu ya
kwanza kwa kutoa dola bilioni 3.8, na ujenzi utafanywa na kampuni moja ya
Kichina.
Ujenzi huo unatazamiwa kuanza mezi Oktoba mwaka huu na
kilometa 610 (maili 380) kutoka pwani kuelekea Nairobi zintakamilika mapema mwaka
2018.
“Gharama za usafirishaji wa wananchi na mizigo kupitia
kwenye mipaka yetu utapungua sana,” amesema Raia wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusainiwa kwa mkataba huo.
Awali Rais Kenyatta alisema kuwa reli hiyo itapunguza
uagizaji wa mizigo kutoka senti 20 za dola mpaka senti 8 kwa kilometa.
Naye Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang, alisema kuwa
mradi huo unaonesha kuwa kuna manufaa kwa pande mbili katika ushirikiano baina
ya China na mataifa ya Afrika Mashirika, na kwamba reli hiyo ni sehemu muhimu
sana ya maendeleo ya miundombinu na usafirishaji katika ukanda huu.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, benki ya Eximbank ya
China itatoa asilimia 90 ya fedha za kugharamia awamu ya kwanza ya ujenzi huo,
huku Kenya ikitoa asilimia 10.
Baada ya kukamilika kwa awamu hiyo, kazi ya kuitandaza
reli hiyo kwenda nchi nyingine za ukanda huu itaanza.
Shughuli ya utiaji saini ilishuhudiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mheshimiwa Bernard
Membe, aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete, Rais Paul Kagame wa Rwanda, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang na marais Uhuru
Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Salva Kiir wa Sudan Kusini.
Ujenzi wa reli ya zamani uliofanywa na wakoloni ulianza
mjini Mombasa mwaka 1895 na kufika Nairobi mwaka 1899.
Ilifika kwenye pwani ya Ziwa Victoria mwezi Desemba
mwaka 1901.
Wakati wa ujenzi huo wafanyakazi wasiopungua 2,000 walipoteza
maisha yao, wengi wao wakiwa vibarua wa Kihindi walioletwa Afrika Mashariki kwa
kazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment