Waziri mkuu wa Ubelgiji anayeshiriki mapenzi ya jinsia
moja, Elio Di Rupo amewasomea viongozi wa Afrika na kuwataka kuheshimu haki za
watu wanaotengwa ikiwemo wapenzi wa jinsia moja.
Alisema ni jambo la kushangaza na lisilokubalika kwamba
watu wanahukumiwa kwa sababu ya wanavyochagua kuishi maisha yao.
Bwana Di Rupo alikuwa anahutubia kongamano la viongozi
wa Afrika na Muungano wa Ulaya mjini Brussels Ubelgiji lililohudhuriwa na
Marais wa Afrika.
Mwaka huu Nigeria na Uganda zilikaza sheria zake kuhusu
mapenzi ya jinsia moja.
Nchini Uganda yeyote anayepatikana na hatia ya kushiriki
mapenzi ya jinsia moja watafungwa maisha jela
Wanaharakati wanaopinga mapenzi ya jinsia moja Uganda
Vitendo vya mapenzi ya jinsia moja vimeharamishwa katika
nchi nyingi za Afrika ambako mapenzi ya jinsia moja yanaonekana kama kitendo
kiovu na kisichokubalika.
Bwana Di Rupo ni afisa wa pili wa ngazi ya juu Ulaya
kutangaza kuwa yeye ni shoga. Waziri mkuu wa Ieceland Johanna Sigurdardottir
pia amejitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja.
"hatuwezi kukubali kuwa baadhi yetu wananyimwa haki
zao na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa wapenzi wa jinsia moja,'' alisema
waziri mkuu huyo.
Rais Museveni na mwenzake wa Nigeria Goodluck Jonathan
hawajajibu kisomo hicho.
Maafisa wakuu wa Uganda wamekuwa wakitetea msimamo wa
Rais Museveni kuhusu sheria yake kali ya mapenzi ya jinsia moja wakisema kuwa
Uganda ni nchi huru ambayo mataifa ya magharibi hayawezi kuishawishi hivi hivi.
Chanzo:BBC
0 comments:
Post a Comment