Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya kutengeneza mifumo ya kompyuta
(software) kutoka Marekani ya Mozilla, Brendan Eich, ametakiwa kujiuzulu mara
moja kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono marufuku ya ndoa za jinsia moja
iliyopitishwa katika jimbo la California nchini humo siku kumi tu baada ya
kuchukua wadhifa huo.
Mwezi uliopita, kampuni hiyo ilikosolewa vikali kwa
kumteua Eich kuwa afisa mtendaji mkuu wake.
Hatua hiyo ya kujiuzulu imekuja baada ya Eich kutoa
msaada wa dola 1,000 mwaka 2008 katika kampeni ya kupinga kuhalalishwa kwa ndoa
za jinsia moja katika jimbo la California.
Mwaka uliopita, marufuku hiyo ilibatilishwa baada ya
Mahakama Kuu ya Marekani kuingilia kati hukumu ya mahakama ya chini.
Mgogoro huo umemfanya mwenyekiti wa Mozilla, Mitchell
Baker, kuomba radhi kwa kitendo kilichofanywa na kampuni hiyo.
"Hatukuchukua hatua ambayo mliitarajia kuchukuliwa
na Mozilla. Hatukuchukua hatua za kutosha kuwa karibu na watu wakati utata huu
ulipoanza. Tunaomba radhi. Tunapaswa kufanya vizuri zaidi,” alisema.
Wakati huo huo, Eich ametoa taarifa akisema kuwa kwa
mazingira yalivyo sasa hawezi kuwa kiongozi mwenye ufanisi.
Katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, Eich alitetea
msimamo wake akisema kuwa ana uwezo wa kutofautisha mambo ya imani yake na
masuala ya biashara anayoiendesha.
Alipoulizwa kama anaweza kujiuzulu, alisema kuwa anaiachia
bodi ndio itoe uamuzi.
"Ninafanya kazi kwa ridhaa ya bodi. Wanaweza kunitaka
nijiuzulu, nami nitakuwa tayari kuukubali na kuupokea uamuzi huo. Mimi bado ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni kwa asilimia mia moja mpaka pale bodi
itakapoamua,” alisema.
Wataalamu wengi wamekosoa hatua ya Eich kuondoka. Bwana huyu
ndiye aliyetengeneza mfumo wa lugha ya kompyuta wa Javascript na ni muanzilishi
mwenza wa kampuni ya Mozilla.
0 comments:
Post a Comment