Mlinda mlango wa vinara wa ligi ya nchini Italia
Juventus, Gianluigi Buffon, amesema kukubali kupoteaa mchezo dhidi ya Napoli
imekua ni pigo kubwa sana kwao, katika mbio za kutetea ubingwa wa Scudeto
kutokana na milango ya kuwania ubingwa huo kunguka tena kwa mahasimu wao AS
Roma ambao wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ya Sirie A.
Gianluigi Buffon, ambae jana alikua langoni mwa Juventus
na kuruhusu kufungwa mabao mawili yaliyopachikwa wavuni na Jose Callejon pamoja
na Marik Hamsik amesema hawana budi kujilaumu wenywe kwa kushindwa kusaka
ushindi katika mchezo huo ambapo hata hivyo amekiri ulikuwa mgumu kwao.
Buffon ambae pia ni mlinda mlango namba moja wa timu ya
taifa ya Italia, amesema kwa hakika Napoli walionyesha mchezo mzuri kuliko
Juventus na walistahili kupata ushindi kama ilivyoonekana katika uwanja wa San
Paolo hiyo jana.
Amesema kila mmoja hakuamini kilichotokea uwanjani hapo,
kufuatia ubora waliokua nao kabla ya mchezo huo, lakini kwa sasa hawana budi
kujipanga upya kwa ajili ya kukabiliana na upinzani mkali kutoka kwa AS Roma
ambao wamewaacha kwa point 11.
Hata hivyo mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 36,
amesema pengo la point 11 huenda mashabiki wao wanaliona ni kubwa, lakini kwake
haamini hivyo kutokana na soka kuwa na matokeo tofauti kila kukicha, hivyo
amewataka waamini kama anavyoamini yeye.
“ Tulistahili kufungwa kutokana na kiwango duni
tulichokionyesha, lakini kufungwa kwetu pia kumetoa nafasi kubwa kwa AS Roma
kuendelea kutukariba katika msimamo wa ligi na hakuna njia mbadala zaidi ya
kuhakikisha tunashinda mchezo wetu ujao” Alisema Gianluigi Buffon.
“Kwa hakika sikushangazwa na matokeo hayo ya kufungwa
mabao mawili kwa sifuri, kwani tulijiamini kupita kiasi, kutokana na mwenendo
wetu mzuri tuliokuwa nao kabla ya kuja hapa Stadio San Paolo, lakini
tumejifunza kutokana na makosa yetu wenyewe, hivyo hatuna budi kucheza
kikamilifu kwa kuhakikisha tunashinda kila mchezo unaotukabili” Aliongeza kipa
huyo ambae ameshaidakia timu ya taifa ya Italia katika michezo 139.
Kufungwa katika mchezo wa jana, kunaifanya Juventus
kumaliza ubabe wa kucheza michezo 22 bila kufungwa msimu huu, na mchezo dhidi
ya Napoli unakua mchezo wao wa pili kufungwa, baada ya kupoteza mchezo wa
kwanza dhidi ya Fiorentina ambao waliibuka na ushindi wa mabao manne kwa mawili
Oktoba 20 mwaka jana.
Juventus kwa sasa wanajiandaa na mchezo ujao ambapo kati
kati ya juma hiili watacheza dhidi ya Olympique Lyonnais kutoka nchini Ufaransa
katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya
barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment