![]() |
| Eneo ilipotokea milipuko ya mabomu katika Ubalozi wa Iran mjini Beirut, Lebanon, Novemba 19, 2013. |
Kwa uchache watu watano wamepoteza maisha na wengine
kadhaa kujeruhiwa katika mashambulizi mawili ya bomu kusini mwa mji mkuu wa
Lebanon, Beirut.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini humo, mashambulizi
hayo yametokea kusini mwa kiunga cha Bir Hassan jirani na Kituo cha Utamaduni
cha Iran na Ubalozi wa Kuwait.
Kikundi cha Brigedi ya Abdullah Azzam kimedai kuhusika
na milipuko hiyo kikisema kuwa kitaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya
maslahi ya Iran na kundi la Hizbollah nchini humo.
Katika miezi ya hivi karibuni, Lebanon imekuwa ikikumbwa
na mashambulizi kama hayo, ambapo idadi kubwa ya watu wamepoteza maisha yao.
Zaidi ya watu 20, akiwemo mwambata wa Ubalozi wa Iran
mjini Beirut, waliuawa na wengine wasiopungua 150 kujeruhiwa mwezi Novemba
mwaka jana baada ya milipuko miwili kupiga jirani na ubalozi wa Iran kusini mwa
mji huo.
Kufuatia tukio hilo, kundi la Brigedi ya Abdullah Azzam lilidai
kuhusika na milipuko hiyo.
Kiongozi wa kundi hilo, Majid al-Majid, alikamatwa
mapema Januari mwaka huu na kufariki dunia siku chache baadaye akiwa gerezani
nchini Lebanon kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kuzorota kwa afya yake.

0 comments:
Post a Comment