![]() |
| Maelfu ya wafanyakazi wa sekta ya umma wakiandamana mjini Pretoria, Afrika Kusini. |
Waandamanaji nchini Afrika Kusini wamefanya ghasia na
kuzichoma moto nyumba kadhaa mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Pretoria
wakapinga kuapndishwa kwa bei za umeme.
Maandamano hayo yamekuja siku moja baada ya mkusanyiko
mwingine katika eneo hilo kugeuka na kuwa wa ghasia, ambapo watu kadhaa
walikamatwa, kwa mujibu wa duru za polisi na za wanausalama.
Polisi wanasema kuwa waandamanaji wanaodai kushushwa kwa
bei za umeme walichoma ukumbi, kliniki na nyumba moja katika wilaya ya Bronkhorstspruit.
Hata hivyo, taarifa ya jeshi hilo inasema kuwa hakuna aliyejeruhiwa katika
matukio hayo.
Hilo ni tukio jipya kabisa katika mfululizo wa ghasia
ambazo huzuka mara kwa mara katika maeneo ya jamii masikini nchini humo ambao
wanaghadhibishwa na huduma duni zinazotolewa na serikali.
Wiki iliyopita waandamanaji walikichoma moto kituo
kimoja cha polisi na ofisi za manispaa.
Wakaazi hao wamekuwa wakilalamika kuwa hawawezi kulipia
gharama kubwa za umeme. Pia wanazilaumu mamlaka kwa kuzimbambikia bili familia
zenye kipato cha chini.
Licha ya kuwa na utajiri wa madini na rasilimali za
kilimo, kama ilivyo kwa nchi nyingi za Kiafrika, nchi hiyo bado imeendelea kuwa
na viwango vidogo vya mishahara kwa wananchi.
Afrika Kusini ina hazina kubwa ya madini mbalimbali kama
vile dhahabu, almasi, urania, makaa ya mawe na mengineyo.

0 comments:
Post a Comment