
Dar es Salaam, 5 Februari, 2014
Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa
kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari 5, 2014. Hii
imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na
nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya
Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.
Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha vituo vyetu vya
kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi juu kushindwa kufanya
kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana kumesababisha kushindwa kutoa huduma
za mawasiliano.
Kutokana na hilo wateja hawakuwa na uwezo wa kupiga
simu, kutumia intaneti na hata huduma za kifedha. Tunatambua usumbufu
ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara nyingine tena tunaomba radhi na
tunashukuru kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho huduma zilikosekana.
Mafundi wetu wameweza kurekebisha uharibifu uliotokea
barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli za ujenzi wa
barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea katika Barabara ya
Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na nyaya zilizo katika mkonga wa
mawasiliano kuungua kulikosababishwa na zoezi la uchomaji taka lililokuwa
linaendelea katika sehemu ambayo mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo.
Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, Tumejidhatiti
katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee wakati wote watakapokuwa
wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna ambavyo wameendelea
kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo yanapojitokeza.
Rene Meza
Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania.
0 comments:
Post a Comment